Tafuta katika Blogu Hii

Jumanne, 27 Februari 2018

RAIS ACHAGUWA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI

Usiku wa jana, February 27,2018 Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa ametangaza baraza lake jipya la Mawaziri ikiwa ni baada ya kuchukua madaraka kutoka kwa Jaco Zuma.

Baadhi ya mawaziri walioteuliwa ni  Nhlanhla Nene aliyekuwa Waziri wa zamani wa fedha. Nene alifukuzwa  kazi December, 2015 na Rais wa zamani Jacob Zuma na nafasi yake ikachukuliwa na Des van Rooyen.
 
Baada anguko la thamani ya randi, Zuma alilazimika kumfukuza kazi Rooyen na kumteua Pravin Gordhan, siku nne baadae ambaye pia alimfukuza kazi baadae. Katika baraza la Ramaphosa, Gordhan amerejea kama waziri wa masuala la biashara.

Jumapili, 25 Februari 2018

 JE UNAZIJUA DALILI ZA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME
Ukosefu au upungufu wa nguvu za kiume ni tatizo kubwa sana ambalo endapo halitatafutiwa ufumbuzi na muhusika linaweza kuyaathiri maisha yake kwa kiasi kikubwa sana. Mwanaume 1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume, hii ni kulingana na utafiti uliofanyika.

Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi. Mwanaume anayekabiliwa na tatizo la ukosefu ama upungufu wa nguvu za kiume huonyesha dalili zifuatazo:-

1. Kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume wake barabara. Kwa kawaida uume wa mwanaume aliyekamilika (rijali ) unaposimama, hutakiwa kuwa imara kama msumari, lakini kwa mwanaume anaye kabiliwa na tatizo hili uume wake hata ukisimama hubakia kuwa lege lege na huweza kusinyaa wakati wowote. Tatizo hili ni matokeo ya kulegea kwa mishipa ya uume. Mishipa ya uume ndio inayo ufanya uume usimame barabara. Mishipa hii inapokuwa imelegea, uume hauwezi kusimama barabara hata iweje.

2. Kukosa hamu ya tendo la ndoa: Hapa mwanaume anakuwa hana uwezo wa kutamani kufanya tendo la ndoa hata anapokuwa faragha na mke wake. Tatizo hili kwa kiasi kikubwa husababishwa na msongo wa mawazo.

3. Kutokuwa na uwezo wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara moja. Hapa mwanaume akishakamilisha mshindo mmoja wa tendo la ndoa basi anakuwa hana tena uwezo wa kurudia mshindo mwingine. Hali hii husababishwa na kutokuwa na msukumo wa damu wa kutosha kwenye mishipa ya kwenye uume.

4. Kufika kileleni mapema

5. Kutokuwa na uwezo wa kusimamisha kabisa. Hali hii hutokea pindi tatizo la kutokuwepo kwa msukumo wa damu wa kutosha kwenye mishipa ya uume, linapokuwa limekomaa. Na wakati mwingine, hali hii hutokea pindi vyanzo zaidi ya kimoja vya tatizo la kiume vinapo kuwa vimejitokeza kwa mtu mmoja.

6. Uume kusinyaa na kurudi ndani. Hapa uume wa mwanaume unakuwa umesinyaa na kurudi ndani. Uume huu unakuwa hauna uwezo wa kukamilisha tendo la ndoa.

Kwa ufupi sana, mambo yafuatayo ndio vyanzo vikuu vya tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume:-
• Upigaji punyeto wa muda mrefu.
• Msongo wa mawazo.
• Ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu (pressure).
• Kupooza kwa mwili.
• Kuugua ugonjwa wa ngiri.
• Kuugua chango la kiume.
• Ulevi uliokithiri.
• Kuwa na wasiwasi wa kumudu kutekeleza tendo la ndoa.
• Woga wa kufanya tendo la ndoa.
• Uzoefu wa kukatisha tamaa wa siku za nyuma.
• Ulaji mbovu wa vyakula haswa vyenye mafuta mengi/kupita kiasi.
• Mazingira yasiyoridhisha wakati wa tendo la ndoa.
• matumizi ya madawa makali (hususani madawa ya kizungu) ya kuongeza nguvu za kiume, husababisha mishipa ya uume kulegea Kutokuwa na mzunguko mzuri wa damu mwilini, hasa sehemu za viungo vya uzazi kwa mwanaume.
• Kutokuwa na kiwango cha kutosha cha homoni ya Testosterone.
• Kupungukiwa protini na hivyo kukosa amino asidi mwilini.
Kutokuwa na nguvu za kiume huleta madhara na athari nyingi sana kwa muhusika. Baadhi ya athari hizo ni pamoja na:-
• Kuvunjika kwa mahusiano ya kimapenzi.
• Kuvunjika kwa ndoa.
• Kujiua: Baadhi ya wanaume hufikia uamuzi wa kujiua baada ya tatizo kuwa kubwa na kutumia dawa za aina mbalimbali bila mafanikio.

HII KALI:Mwanamke aomba mbegu za mwanaye wa kiume aliyefariki
Nchini India mwanamke mmoja ajulikanaye kwa jina la Rajashree Patil, 49, ambaye miaka miwili iliyopita alifiwa na mtoto wake wa kiume wa pekee aliyekuwa anaumwa saratani ya ubongo.

Kutokana na kushindwa kumsahau mwanaye na kukubaliana na ukweli wa kuishi maisha bila mwanaye huyo mama huyo aliamua kwenda kuomba mbegu za kiume za mwanaye huyo ambazo zilikuwa zimehifadhiwa hospitalini.

Alimtafuta mwanamke mmoja na kumuomba amlipe ili apandikizwe mbegu hizo  za mwanaye na ashike ujauzito (surrogate) ili tu amzalie wajukuu ambao anaamini wataziba pengo la mwanaye huyo.

Habari njema ni kwamba mwanamke huyo amefanikiwa kujifungua watoto mapacha siku za hivi karibuni. Pacha hao ambao ni wa kike na wa kiume wamepewa majina ya Prathamesh na Preesha.

Jumamosi, 24 Februari 2018

MAJIMAJI BILA WACHEZAJI WAO SABA KESHO DHIDI YA YANGA,MAMBO NI MOTO
kikosi cha Majimaji kitakuwa na ukosefu wa wachezaji 7 watakaoikabili Yanga, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho siku ya kesho,

Kocha wa timu hiyo, Habibu Kondo, amesema timu hiyo watalazimika kutumia kikosi cha pili ili waweze kupambana na yanga, baada ya kuwakosa wachezaji hao.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kondo amesema wachezaji hao wamepumzishwa kutokana na masuala mbalimbali ya kinidhamu kuwakabili.

"Itatubidi tuingize wachezaji watano wa kikosi cha pili, sababu katika kile cha kwanza, jumla ya wachezaji saba hawatokuwepo" alisema Kondo.

Unywaji wa Chai ya moto husababisha saratani ya koo

Wanasayansi nchini China wamefanya utafiti na kugundua kuwa unywaji wa chai ya moto mara kwa mara unaweza kusababisha saratani ya koo.
Kwa mujibu wa makala iliyochapishwa katika jarida la Annals of Medicine Internal, hali ya afya na tabia ya kula ya watu 456,155 kati ya umri wa miaka 30-79 ilichunguzwa wakati wa utafiti huo.
Utafiti umefanywa ndani ya miaka kumi.
Imebainika kuwa watu amabo hunywa mara kwa mara chai ya moto au gramu 15 za pombe wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata saratani ya koo,mara tano zaidi ya asiyekunywa.
Na kwa wavuta sigara,kuna uwezekano wa wao kupata ugonjwa huo mara mbili ya mtu asiyevuta sigara.

Ijumaa, 23 Februari 2018

ZITTO KABWE CHINI YA MIKONO YA POLISI

Mbunge wa Kigoma Mjini na Mwenyekiti wa taifa wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe jana  February 22, 2018 ameshikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo cha Polisi cha Mgeta wilayani Mvomero, Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya mahojiano.

Zitto kwa sasa yupo katika ziara ya mikoa mbalimbali kwa ajili ya kukagua na kuimarisha uhai wa chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari jana alhamisi February 22,2017 amesema ametakiwa kuripoti katika kituo hicho baada mkuu wa polisi wa wilaya (OCD) kuagiza aende.

"ninapozungumza na nyinyi naelekea kituo cha polisi na gari yangu ipo mbele ya polisi na sijajua kosa langu ni nini" amesema Zitto.

Waandishi wa habari walipo jaribu kuzungumza na Katibu Kamati ya Uenezi na Mawasiliano ya Umma  wa ACT Wazalendo Ado Shaibu alisema mpaka sasa bado yupo anashikiliwa na Polisi hawajui ni kosa gani ambalo Zitto Kabwe limefanya akamatwe.

Nae Wakili wa Zitto Kabwe, Emmanuel Lazarus Mvula alisema jalada la mashataka dhidi yake limefunguliwa katika kituo cha Polisi Mgeta. 

“Hivi Sasa saa 3.30 usiku ndugu Zitto amechukuliwa na OC-CID na polisi wenye silaha anapelekwa Kituo cha Polisi cha Wilaya, cha Dakawa ili kuandika maelezo kwasababu hakuna umeme katika kituo cha Polisi Mgeta”



 Baada ya kifo cha AKWILINA Sheria inasemaje kwa vifo kama hivyo

Baada ya tukio la kupigwa risasi na kufariki mwanafunzi wa chuo cha NIT Akwilina Akwilini wakati wa maandamano ya CHADEMA licha ya kwamba yeye hakuwa kwenye maandamano hayo, tumemtafuta mwanasheria Jebra Kambole ambaye ameeleza kuhusu sheria inasemaje endapo vinatokea vifo vya aina hiyo..?

Mwanasheria Jebra Kambole amesema kwamba sheria inatoa muongozo kwamba kimsingi jeshi la polisi lina mamlaka ya kufanya uchunguzi aidha linajichunguza lenyewe au linachunguza kitu kingine na wakishajua nani amefanya kosa atachukuliwa hatua za kisheria.
SHILOLE ASEMA KUMPIGA MAKOFI MPENZI WAKO NI MAHABA NIUWE
MSANII Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ambaye ameolewa hivi karibuni na mzee baba Uchebe amesema katika maisha yake ya ndoa na mumewe Uchebe hajawahi kumpiga makofi.

Kauli hiyo Shilole aliitoa juzi alipofanyiwa mahojiano na Enews ya EATV ambapo aliulizwa kama atampiga makofi mumewe kama alivyofanya kwa wanaume waliotangulia kabla ya kuolewa.

“Tabia hiyo nimeacha na ule ulikuwa utoto siwezi kumpiga Uchebe kwani ni mwanaume anayejiamini na jasiri pia ana misimamo yake”.

“Nikimpiga yatakuwa makofi ya chumbani ambayo mtu na mpenzi wake wanafanya kimahaba, si unajua yule alikuwa anapigana (bondia) na ana mkanda,” aliongeza Shilole.

Shilole aliwahi kumpiga makofi aliyekuwa mpenzi wake Nuh Mziwanda kabla ya kuachana.

Alhamisi, 22 Februari 2018

 Wafanyakazi wa Chuo kikuu mbaroni
Idara ya Uhamiaji nchini inawashikilia watanzania 9, ambao ni  wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala(KIU) jijini Dar  es Saalam kwa kutokuruhusu maofisa wa idara uhamiaji kufanya kazi yao walipofika chuoni hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari Msemaji wa  Idara ya Uhamiaji Ally Mtanda amesema watu 9 washikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kuzua chombo kinachohusika na uhamiaji wasitimize adhima yao.

"Watu hao baada ya maofisa wetu jana kufika pale KIU waliamua kuwazuia kwa kufunga milango ili tusipate nafasi ya kufanya kile ambacho kimetupeleka,"amesema.

Kukamatwa kwa watu hao kunafanya idadi ya wanaowashikiliwa na Idara ya Uhamiaji kufikia 48.

"Idara ya Uhamiaji inaendelea kuwahoji na kati ya hao wanaoshikiliwa wapo raia wa Nigeria watano, raia wa Congo mmoja, raia wa Uganda 30, raia wa Kenya 3 pamoja na hao raia wa Tanzania 9,"amesema.
Amefafanua Idara ya Uhamiaji itaendelea kukagua vyuo mbalimbali  nchini kwani ni agizo la Wizara ya Elimu, Sayansi na  Teknolojia.
Simulizi ya kweli kuhusu madhara ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile
Nimeolewa nina mtoto mmoja, mme wangu anapenda sana kushika shika makalio yaani akiona niko mtupu tu basi bora anishike hata makalio aridhike, sikuogopa nilijua mwili wangu ni haki yake nikawa namuwachia, tukilala tu, anaweka mkono kwenye makalio ndio usingizi unampata alizowea hivyo.

Yaani hata tugombane vipi tukilala tu anaweka mkono wake kwenye makalio kwa juu kila nikishtuka nakuta mkono, ILA HAKUWAHI KUNIAMBIA HABARI ZA KIINGILIA KINYUME CHA MAUMBILE

Aliniheshimu sana wala hata sikuwahi kuhisi kama ana mtu nje yaani hata wazo sikuwa nalo maana unawezashinda na simu yake usione chochote, hata upekuwe vipi hukuti chochote, saa moja yupo nyumbani, weekend hatoki, yaani amani tupu, sasa kuna kipindi.

AKAANZA TATIZO LA KUTOSIMAMISHA
Ikawa akifika asubuhi anakuwa ha hamu kabisa, naamimi nakuwa na hamu sana, lakini inakuwa imesimama kidogo sana,basi naichezea naigusisha baadae kabisa ndio inasimama anaingiza, akiingiza unakuta katikati ya mapenzi inalala tena kwahiyo nakuwa sijakojoa yeye analalamika tu anaumia sana hasa sehemu za korodani.

Basi ilichutukua kama wiki kwa hali hiyo nikawa najitahidi kumset mind yake kuwa free nikawa namuuliza labda hali hii iliwahi mpata ujanani akasema hapana, nikawa namuuliza sasa inakuwaje unawaza nini isijekuwa una mawazo, akasema hapana sina mawazo nikamwambia haya niambie basi nini shida, twende hospitali akasema kesho nina dr, rafiki yangu Aga khan nitakwenda kumuona, basi ikaisha.

Kesho yake akaja na dawa kama ungaunga kwenye kakopo, nikamuuliza hii dawa ya hospitali kweli?

Akasema hapana kuna staff mwenzangu nae tatizo hili lilimpataga akanywa dawa hii ya kimasai, unamix na maji ya moto, alikunywa kichupa kile aliuziwa 120,000 alikunywa kikaisha uwezo wa kusimama ulikuwepo, lakini hafiki mwishoni inalala kabisa inakuwa ndogo.

Nikauliza au ni ngiri? akasema hapana.

Hali iliendela hivyo kuna siku nilishtuka sana nilikuwa nafua chupi nikatoa nimfulie na yeye, nikakuta vitu kama usaha umejaa kwenye chupi yake nilishtuka sana sikufua nikaiweka pembeni, nikamsubiri aliporudi nikamuliza huko chini unatoa nini?

Mimi ni mke wako natakiwa kujua uume wako unatoa nini maana ni mali yangu na haki yangu kwanini unaniogopa hata kama unaumwa tena ni vizuri mkeo akijua ajue anakuhudumiaje, niambie kweli, akasema mie sijui, naona tu kuna vitu vinatoka vyamoto vyeupe nikamuuliza vimeanza lini, akasema siku ya tatu leo.

Nikakumbuka kweli siku hizo zote chupi zake alifua mwenyewe nikamwambia sasa kwanini husemi, unakaa kimya, isijekuwa magonjwa ya zinaa akasema niyaote wapi mke wangu, nikamwambia twende hospitali aligoma kwenda na mimi, nilimsimulia rafiki yangu akaniambie niende nikapime mimi maana ushirikiano mme hana.

Nilienda regency nikapima nikaambiwa niko salama salmin sina chochote kile isipokuwa kuna kigozi waliniingiza wakasema kesho yake nifate majibu, nilirudi nikaambiwa kipimo kile pia kinaonyesha niko mzima nikasema asante Mungu.

Ilienda hivyo niliamua kumuacha maana hataki kushirikiana na mimi kabisa.

Kila nikiuliza anaficha ficha siku hiyo usiku nimelala nikasikia mtu analia, nikaamka nikakuta analia huku ameshika nyeti zake analia kwa uchungu sana.

Nilitazama saa ilikuwa saa sita, mie huwa siwezi kuendesha usiku, nikamuita rafiki yake akaja tukampakie hao hadi agakhan njia nzima analia hawezi hata kukaa wala kukunja kiuno yaani ilibidi nikae nyuma na yeye anilalie analia kama matoto, kwa mara ya kwanza nilishuhudia machozi yake na sauti ya kilio
nikajikuta namhurumia nalia na mimi.

Akaniambia mke wangu nishike huku, nipuulize, naumia nishike shike mama naumia analia sana, nikamwambia niambie basi.

Kama uliiba mke wa mtu twende ukaombe msamaha, ona sasa hueleweki unaamua nini, wakati huo imesimama mishipa yote imeonekana kuvimba yaani niliogopa sana, nilimvisha bukta laini tu maana chupi ingemuumiza sana.

Tulipokelewa akaingizwa kwa Daktari cha ajabu kufika pale akawa anataja jina la daktari anaemtaka yeye wakasema hayupo akanipa simu akaniambia chukua namba jina limeandikwa dokta...........................(jina la dokta kapuni yeye kataja mimi admin nimelificha) akasema yeye ndio anajua issue yangu, nikasema issue gani?

Akasema wewe mwambie huyo, wakati nataka kumpigia rafiki yake akasema mwambie hapatikani, anaficha nini huyu jamaa katika hali hii, nikamfata nikamwambia hapatikani yeye analia tu, yule dokta, mwingine akasema acha nikuhudumie mimi.

Akaingia nae chumba cha daktari, sijui ilikuwaje baadae nikaona tu anavutiwa kwenye kitanda anapelekwa wodini, nikaambiwa analazwa, dokta akaniita ofisini akaniuliza huyu ni nani yako, nikasema mme wangu.

Akasema okay, wa ndoa? nikasema ndio, akauliza mna watoto nikasema ndio, akasema okay wangapi, nikasema mmoja wa mwaka mmoja akasema okay, sasa wewe ni mtu mzima ukae hapo na naomba unijibu maswali yangu vizuri ili nijue nakusaidiaje, usiogope usinionee aibu, wewe na mumeo huwa mnafanya mapenzi kinyume na maumbile?

Nilishtuka nusu nianguke kwenye kiti, nikasema nini dr? akasema nakuuliza huwa anakufanya kinyume na maumbile? nikasema no akasema ugonjwa alionao umekuwa sugu na inaonyesha ni mchezo wake wa siku nyingi sana hadi kufikia hatu mbaya hivi.

Nikaanza kuvuja jasho, mwili ukaishiwa nguvu macho yakanitoka vinyweleo vikanisimama dr, aliona hali yangu imebadilika ghafla akaniambia tulia nijibu ili nikupime na wewe yawezekana unaumwa, haiwezekani hali hii iwe hivi kwake wewe ukawa mzima, nikasema no mimi hajawahi kunifanya nyuma wala kuniomba hiyo kitu.

Daktari naapa kwa Mungu mmoja na nimepima juzi juzi tu niko salama, akasema naomba nikupime na mimi, sikubisha akanipima, wakati vipimo vinashughulikiwa nikawa namuuliza sasa mme wangu mwisho wake unakuwa nini.

Akaniambia wagonjwa wa hivi tunawapokea sana siku hizi, sijui huu mchezo wameutoa wapi hata kuvaa condom wanasahau, hawajui madhara yake na ukiwaambiwa hawakuamini, sasa huyu wako kuna kipimo nimechukua, na pale tuliharibu wakati anaumwa hakutakiwa kufanya wala kujaribu hata kidogo alitakiwa apate matibabu mapema bila kufanya chochote kile mishipa imeziba, uchafu umeingia kwa ndani, kwahiyo watamfanyia operation ya kumpasua ili kusafisha na akitoka hapo uwezekano wa kupona ni mkubwa ila uhakika wa kusimamisha ni mdogo sana wamfanyie operation.

Nikasema dr kweli unahikia ni kwa ajili hiyo? akasema niko kwenye hii kazi zaidi ya miaka kumi, jinsi kulivyo na vinavyotoka ni dalili mojawapo kabisa hata sijachukua majibu ya vipimo, ila tulia, usimharakishe na maswali huyu anatakiwa kufanyiwa operation usiku huuhuu, hali yake sio nzuri, niliishiwa nguvu nilitamani nimfate kule chumbani nikamuulize huwa unamuingilia nani?

Kivile niliogopa sana nikaanza kulia sana nawaza anapasuliwaje halafu inakuwaje, nililia sana lakini shemeji yangu alinipa moyo kwamba tumuombee, niliomba tu mungu amsamehe ila amponye.

Sisi tulikuwa nje kwenye gari yaani sikuwa sawa kabisa, wakaanza kumuandaa hadi kufika saa kumi na mbili wakamuingiza kumfanyia, akatoka mida ya saa tatu.

Hajielewi kabisa, akalazwa, nikaitwa nikawa naelekezwa namna ya kumuhudumia.

Ilinipa ugumu sana kuwataarifu wengine maana wangejua kilichotokea kwake nikasema sisemi kwa mtu yeyote kama mme wangu anaumwa hata kwa mama yake sisemi ntauguza peke yangu akinifia tutajua mbele ya safari.

Hata rafiki yangu sikumwambia, ila yule shemu wangu niliwambia asiseme kokote nashukuru hadi leo hii sijasikia kokote.

Niliuguza mgonjwa wangu akapona kabisa ila aliambiwa haruhusiwi kufanya awe anatumia dawa na anarudi hospitali ili kuchekiwa akiwa tayari ndio watamwambia.

Nilishindwa kuvumilia kurudi hadi home ndio niulize, nikamuuliza hospitali, wewe unajua unaumwa nini, akasema ndio mke wangu ni uchafu umeziba nikamuuliza.

Jalala hilo? sema kinyesi ndio kimeziba ya hao unaowawafanya, sasa unaruhusiwa leo nakurudisha kwako salama salmin nakuacha mzima kabisa naondoka na mwanangu.

Siwezi kuishi na wewe hadi useme unamfanyaga nani?

Akasema hakuna kitu kama hicho, akakomaa nikasema poa dr, muongo, tuliruhusiwa hao hadi nyumbani, kufika nyumbani alijua natania, nilimuogesha mwanangu nikamwambia dada ajiandae, na mabegi ya nguo nikachukua funguo zangu, hao kwenye gari, nikamwambia naondoka.

Ukitaka nirudi sema kweli ulikuwa unamfanya nani, niliwasha gari na kuondoka zangu na mwanangu na dada wa kazi.

Nilikwenda kijichi kwa rafiki yangu, alipiga sana simu yangu sikupokea baadae mama yake akaanza kunipigia nikamwambia mama muulize sababu ya mimi kuondoka mwambie aseme mwenyewe kwako, mimi sisemi na niko serious, kweli sikusema nikakata simu, usiku kama saa nne akanipigia simu akasema yuko tayari kusema kweli, nirudi nikamwambia nitakuja asubuhi akakataa akasema nirudi usiku ule ule nikasema siwezi drive usiku mimi, akasema nichukue tax atalipa.

Nilizima simu nikalala kwa rafiki yangu asubuhi akapiga tena, nikaenda niliacha watoto na dada huko kijichi, nilipofika tu nikamkuta kaka peke yake, akaanza kulia anasema nimsamehe, mateso aliyopata huyu bwana yalimtosha alikua akikojoa kwenye mrija ulioingizwa huko chini, alikuwa analia kama mtoto, yaani alikonda ndani ya wiki alikuwa anateseka akianza kukojoa ananiita ananishika kwa nguvu anang'ata meno ndio anakojoa aliteseka vya kutosha aisee hadi nilimuhurumia.

Basi nilivyoenda akaanza kulia mke wangu nisamehe nikamwambia niambie uli**** nani akanitajia ni dada mmoja hivi, mfanyakazi wa bank(jina kapuni by admin).

Nikamuuliza ulianza lini?

Akasema siku nyingi, naomba nisamehe nilianza kabla sijakuoa hata wewe, ilia niliapia mke wangu nitamheshimu sitamvunjia heshima, ndio maana niliamua kufanya huko, nikamwambia uliniheshimu asante lakini hukuogopa magonjwa? heshima iko wapi hapo, je tungekutwa tumeathirika ungeniambia nini? mie mwenzio nishapima kila kitu mzima, haya wewe umepima? akasema nisamehe kwanza hatarudia na akirudia niondoke nilimhurumia kwakuwa nampenda sana, nikasema namsamehe na aibu nitamfichia ila huyo mwanamke nitamtafuta nimwambie tu aache.
Nilikubali kumsamehe kwa sharti la kutofanya chochote hadi akapime kwanza.

Tulikwenda hadi hospitali akapima alikutwa negative, wakati anajisubiria maana alikatazwa sex kabisa kwa kipindi hicho, utulikaa miezi mitatu bila kufanya chochote kile, tukarudi tena hospitali wakapima yuko negative, tukarudi home bado hakuruhusiwa kusex, ilifika miezi mitano kasoro nikaitwa na yeye hospitali tukaelekweza how can we sex kwa kipindi cha mwanzo kutuokana na hali yake.

Ilichukua muda sana kufanya kawaida mwanzoni alikuwa anaishia njiani au hakojoi kabisa, niliambiwa kwa upande wao madokta wamemaliza jamaa yako fresh kazi ni kwangu kumuandaa, kumuweka sawa ili aperform maana imeathiri hadi kichwa chake, nilikuwa na hasira sana mwanzoni, mwisho nilimhurumia kwakweli maana nampenda, nikawa najitahidi kumpa upendo wangu wote,namuweka karibu sana.

Ilisaidia sasa hivi yuko vizuri tunaenda kama kawaida na sasa niko na mimba, ya miezi mitano.

Back to the lady from bank,

Nilifunga safari hadi ofisini kwao, nikamuulizia nikamkuta, akaja kuniona, kabinti kazuri huwezi kuamini admin mdogomdogo mzuri sana anaonekana mstaarabu sana nilishangaa yeye ananijua mimi simjui, alishtuka kuniona nikahisi, ananijua nikamuuliza do you know me? akasema no oh yess nikamwambia yes or no! akasema yes ni mrs...................... nilishikwa hasira hapo hapo nilimuwasha kibao paaaaa!

Waliokuwepo karibu waliona, yule dada mwenyewe akanishika mkono tukaongelee nje maana wengi walikuwa hawajashtukia kila mtu yuko busy, waliona wachache waliokuwa karibu ila kuna staff mwenzie aliona.

Nikamwambia kwanini umemtesa hivi mme wangu, kwanini unampa makalio wako mchafu mme wangu hadi kummpa matatizo makubwa vile, kwanini usitulie ukapata wako mbona wewe bado mdogo sana, wakati tunaongea akawa anasema dada naomba tuongee jioni hapa ofisini watasikia nikamwambia nikitoka hapa naingia kuonana na bosii wako.

Nimwambie kaajiri mashetani humu, akatoka mdada mwingine, sie yule alietuona, akamuuliza .................... vipi kwema?

Nimeambiwa nitoke nje kuna mtu amekupiga nani? akasema hakuna alienipiga, nikamwambia mimi nimempiga njoo ujue sababu, yule binti nusu akimbie, akaniambia niko chini ya miguu yako naomba tuongee baadae.

Mwenzie akaja akaniuliza chanzo nikamwambia aseme mwenyewe binti alilia kama kapokea msiba, anasema tu nisamehe nitakutafuta nikamwambia.

Jioni unitafute mwenyewe ikibidi njoo kwangu maana unapajua, jiulize hapa nimefikaje, jina nimepataje, mnasahau kuwa hampendwi nyie mnachezewa tu, tazama sasa karudi kwangu kwa heshima na adabu zote, nimempokea mikono miwili, kanielekeza hadi kwenu hadi unapoishi hadi wazazi wako nimeelekezwa umeharibiwa makalio hayo, mie wangu uko na adabu zake namuhurumia atakaekuja kukuoa... nitafute mwenyewe, niliondoka kwa hasira sana nikaanza kulia kwenye gari, kweli alinipigia saa kumi na mbili akiulizia kama tunaweza kuonana sehemu nyingine sio nyumbani, nilikuwa na hasira nikasema nitamuua nipate kesi, nililia sana niakamwambia nitakutafuta niko mbali, sikumtafuta kama wiki hivi yeye ndio alikuwa akinitafuta na kunitext sms za kuomba radhi nimfichie ufirauni wake.

Niliingia kwenye maombi, nikaomba sana mungu anisamehe nami nawasamehe walionikosea, nilimwambia yule binti kwamba basi nimemsamehe, mme wangu nilisamehe, hadi leo niko nae.

TAKUKURU YATOA TAMKO KUHUSU KESI YA MALINZI
Leo mbele ya Hakimu Mkazi Kisutu TAKUKURU imetoa tamko mbele hakimu kwamba hawacheleweshi kwa makusudi kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili aliyekuwa Rais wa (TFF), Jamal Malinzi na wenzake bali jalada lipo kwa DDP na anasubili kibali cha usikilizwaji wa kesi maneno haya aliongea wakili wa TAKUKURU,leornad Swai kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

Hata hivyo, Wakili wa utetezi Abraham Senguji amedai ni miezi 8 hadi sasa Jamal Malinzi yupo gerezani, hivyo anaomba upande wa mashtaka uharakishe upelelezi.

Swai amesema hawacheleweshi upepelezi wa kesi hiyo bali jalada lipo kwa DDP analipitia hivyo anaomba kesi iahirishwe hadi tarehe nyingine . 

Baada kueleza hayo, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi March 1,2018 kwa ajili ya kutajwa.

Mshitakiwa anakabiliwa na kesi ya utakafutishaji fedha na mashtaka mengine 28
 Alichokifanya Zitto Kabwe NI MFANO wa kuigwa na viongozi wetu
Siku ya leo wakazi wa kata ya Tomondo wilayani Morogoro jimbo la Morogoro kusini Mashariki mambo yao ni motoooo baada ya kupata ufumbuzi wa baadhi ya kero za miradi yao mbalimbali ya maendeleo

Kata hiyo inayoongozwa na Diwani wa Chama cha ACT Wazalendo, Hamisi Msangule February 21, 2018 ilitembelewa na viongozi wa chama hicho ngazi ya Taifa, Mkoa na Jimbo ambao waliwezesha kutatua baadhi ya changamoto.

Changamoto kubwa ambayo imepewa kipaumbele kutatuliwa na chama hicho ni kero ya maji inayowakabili wakazi wa kata hiyo ambayo chama hicho kimeahidi kuwapeleka wataalamu wa kutoboa visima virefu kwenye kila Kijiji ndani ya mwezi huu.

Akiwa kwenye kikao cha ndani na wananchi wa kata hiyo mwenyekiti wa chama cha ACT kitaifa , Zitto Kabwe aliwaambia wananchi hao kama watashindwa kumaliza kero hiyo haitakuwa na maana tena chama hicho kupewa dhamana tena kuongoza.

“Chama chetu ni tofauti sana na vyama vingine, tunafanya siasa za maendeleo kwa ushirikishaji wananchi katika kutatua changamoto zao,” -Zitto Kabwe

Jumatano, 21 Februari 2018

ZARI APATA KIBOKO YA DIAMOND PLATNUMZ

IIkiwa ni siku chache tokea mama Tifah, Zari Hassan aachane na chibu di chibude, Diamond platnumz aka simba baada ya kuchoshwa na tabia ya mpenzi wake ya kutoka na wasichana wa kila aina

Inasemakana Mama Nillan amepata mpenzi mpya wa kutuliza maumivu yote aliyopata kwa Diamond platnumz, kwa tetesi za chini chini boyfriend mpya awadhifa mkubwa kuliko mzee baba simba na kwamba anamiliki mgodi wa dhahabu afrika kusini na sasa yupo kwenye harakati za kumuhamishia mtoto mzuri Zari ulaya ili asahau shida zake

MKUU WA WILAYA AMRUHUSU MUMEWE KUOA MKE WA PILI
Leo watumizi wa mitandao ya kijamii walipigwa na bumbuwazi baada ya kuona post iliyo kwenye ukurasa wa instagram (@zainabuabdallah93) ya Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainab Abdallah akitoa pongezi kwa Mume wake baada ya kuoa mke wa Pili. Watu wengi walijikuna sikio huku wakibakli mdomo wazi, kwani ni nadra sana kuonaMwanamke mwenye cheo kikubwa na wadhifa wa kutosha akimpongeza Mumewe kwa kuongeza mke

Kupitia ukurasa wake wa instagram mkuu wa wilaya ya pangani ameandika 
kuwa wazo la mume wake kuongeza mke wa pili lilitoka kwake, baada ya kuona majukumu ya kazi yanambana na kushindwa kutekeleza majukumu ya ndoa.

Nichukue nafasi hii kumpongeza Mume wangu  kwa kuongeza mke wa pili. Kwa kuwa dini yetu ya Kiislam inaruhusu, wazo la kufanya hivyo lilitoka kwangu, kulingana na uzito wa majukumu yangu nalazimika mda mwingi kuwa mbali na nyumbani na hivyo mume wangu kukosa huduma za msingi” -DC Zainab 
”Namshukuru kwa kunielewa na kulifanyia kazi ombi langu, hatimaye nimempata mwenzangu wa kusaidiana naye majukumu mazito ya ulezi wa mume. Alhamdulillah, M/Mungu ametupa riziki na uwezo, hivyo tunapaswa kutumia neema hizi na wengine. Mavazi ya mume wangu nimeyaandaa mwenyewe, yaa rabb atupe stara inshaaAllah.” DC Zainab

Madhara ya kupiga punyeto kwa wanaume

Tunahitaji mahusiano ili tuongezeke na hili haliwezi kufanikiwa bila kushiriki tendo la ndoa kati ya watu wa jinsia mbili tofauti.
Hisia hizi huanza kujitokeza pale mtu anapofikia wakati wa kubarehe. Hapa ndiyo wakati mgumu na mbaya kwa kijana hasa kwa asiyejitambua na asiye na usimamizi wa karibu wa wazazi au walezi.

Ni wakati huu ndipo mbegu za kiume (manii) huanza kuzalishwa katika mwili wa kijana wa kiume na kupelekea kuanza kuona hitaji la kuwa na mchumba au hata mke.

Kutokana na maisha na tamaduni zetu wa afrika zilivyo hapo ndipo kijana huona hana namna zaidi ya kujichua pale anapokuwa hana mtu wa kujamiiana naye ili kupunguza hamu zake. Kitendo hiki kimeathiri sehemu kubwa ya jamii.
Kupiga punyeto au kujichua hujulikana pia kwa Kiingereza kama “Masturbation”, ni kitendo ambacho huleta matatizo makubwa ya muda mrefu ambayo muathirika huchelewa sana kuyatambua.
Tuangalie sasa madhara 21 yafuatayo ambayo ni matokeo ya kujichua kwa mwanaume:

Madhara ya kupiga punyeto kwa wanaume
1. Punyeto hukufanya uwe dhaifu, inapoteza protini na kalsiamu ndani ya mwili wako.
2. Huleta matatizo kwenye neva nyurolojia ndani ya mwili
3. Ni moja ya kisababishi kikuu cha uhanithi (uume kushindwa kusimama)
4. Ni rahisi kuwa mtumwa wa kujichua (teja) unaweza kujaribu mara 1 tu na tayari ukawa teja wa jambo hilo kila mara
5. Huleta uchomvu sugu na kwa haraka zaidi, mara nyingi utahitaji kulala usingizi hata nyakati za mchana
6. Husababisha mfadhaiko (stress) kwenye akili na kwenye roho yako pia
7. Huleta matatizo ya kisaikolojia, hukusababishia majonzi na huzuni na kukufanya kujilaumu nafsi mara baada ya kumaliza kujichua
8. Punyeto haifanyiki kirahisi, unahitaji akili yako iwaze au itazame picha mbaya au chafu au kumfikiria kimapenzi mtu asiyekuwepo hapo ulipo. Hili ni jambo baya zaidi kwa afya kwani picha hizo hazikuondoki haraka kichwani mwako tofauti na ukishiriki tendo la ndoa na binadamu mwenzio moja kwa moja.
9. Punyeto inakupelekea kufanya makutano haramu kwakuwa hiyo hamu yako ya kutaka kujichua kila mara itakupelekea kuanza kutafuta vijarida au picha za ngono jambo ambalo ni baya zaidi kwa afya yako ya mwili na roho
10. Punyeto inapelekea tatizo lingine kubwa zaidi nalo ni kuwahi kufika kileleni utakaposhiriki tendo la ndoa na mwenza wako, hii itakuletea shida kwenye mahusiano yako wewe mwenyewe na hata kwa mwenza wako.
11. Punyeto inapunguza uwingi wa mbegu (reduces your sperm count) kama matokeo yake mwanaume hataweza kumpa mwanamke ujauzito. Hili la kuwa na mbegu chache ndilo chanzo kikuu cha ugumba kwa wanaume na ni matokeo ya kupiga punyeto mara kwa mara.
12. Kimaadili kabisa punyeto au kujichua ni jambo baya, unamuwaza fulani na kujikuta ukishiriki tendo la ndoa peke yako. Hii inapunguza thamani yako na nidhamu kwa wengine. Unaweza kuwa mzuri kwenye maeneo mengine mengi lakini utaishia kuwa na matatizo kama hutaiacha tabia hii haraka.
13. Punyeto inapoteza muda wako na kukufanya mtu usiye na faida
14. Raha ya kujichua haibaki akilini kwa kipindi kirefu kama vile ukishiriki tendo la ndoa kwa na mtu halisi
15. Punyeto husababisha ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu, ni vigumu kuwa na akili ya utulivu na kukumbuka vitu kama tayari umeshakuwa teja wa punyeto.
16. Kujichua siyo soluhisho la mwisho la hitaji lako, yaani hutaona kuridhika katika kitendo hicho, kadri unavyofanya ndivyo unavyoendelea kuhitaji zaidi na zaidi mpaka mwisho unakuwa hanithi kabisa bila kujitambua
17. Punyeto haina faida yoyote kwenye maisha yako ya kimapenzi, huhitaji kwa ajili ya chochote
18. Punyeto inaongeza aibu, inapunguza uwezo wa kujiamini. Wengi waliozoea kujichua hata kutongoza kwao huwa ni kazi kubwa mno kiasi wengine huona bora kuendelea kujichua kuliko kutongoza mwanamke.
19. Utapoteza hamu ya kushiriki tendo la ndoa kirahisi zaidi kama utaendelea kujichua
20. Punyeto huchochea mapenzi ya jinsia moja hasa mashuleni, vyuoni na kwenye mahoteli na mwishowe hupelekea kusambaa kwa magonjwa mengi ya zinaa.
21. Punyeto inamaliza nguvu za kiume, kama unapenda kujichua basi sahau kuwa na nguvu za kiume. Upungufu wa nguvu za kiume ni janga la kitaifa miaka ya sasa lakini chanzo kikuu ni vijana wengi wa kiume kuanza kujichua tangu wakiwa mashuleni.

Je ufanye nini ili kuacha punyeto au usishiriki mchezo huu mchafu?
Kama muda na umri haukuruhusu kuwa na mke au mchumba, basi fanya yafuatayo:

•Kama bado unasoma kuwa bize na masomo na ujiepushe na makundi hatarishi.
•Jishughulishe na mazoezi ya viungo kila siku. Hii itauchosha mwili wako na hivyo hutapata muda tena wa kujichosha zaidi kwa kujichua kwani tayari utakuwa na uwezo wa kupata usingizi mtulivu sababu ya mazoezi
•Usikae peke yako muda mrefu bila kuwa bize na shughuli yoyote. Kichwa kitupu ni nyumba ya maasi mengi.
•Epuka vyakula vyenye mafuta mengi
•Tumia muda ambao huna kazi kwa kulala na hivyo utakuwa unaipumzisha pia akili yako
•Usikae muda mrefu maeneo kama ya bafuni au chooni
•Usipende kujishikashika na mkono wako sehemu zako za siri wakati wowote.
•Tafuta watu walioathirika na punyeto wakusimulie matatizo wayapatayo kama matokeo ya kujichua. Hii inaweza kukusaidia kuongeza juhudi kuachana na hiyo tabia.
•Futa picha zozote chafu iwe kwenye simu au computer yako na usitembelee blog au tovuti yoyote yenye picha hizo, kama upo kwenye magroup ya namna hiyo kwenye mitandao ya kijamii basi jiondowe haraka iwezekanavyo.
•Kama tayari umeshaoa basi ni dhambi kubwa sana kuendelea kupiga punyeto, utaishiwa nguvu na unaweza kukosa kumpa ujauzito mkeo siku za usoni.
Tambua hakuna dawa ya kuacha punyeto, usije ukaibiwa pesa zako bure, dawa ni kuoa tu.
YANGA WANA SHUGHULI PEVU DHIDI YA ST LOUIS KATIKA LIGI YA MABINGWA LEO

KIKOSI cha Yanga, leo Jumatano kitaingia uwanjani kupambana na St Louis ya Shelisheli kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Klabu Bingwa Afrika, wakati huo huo nyota wake wanne wa kigeni hawatacheza mechi hiyo kutokana na majeraha

Kwenye mchezo huo wa kukata na shoka, Yanga itamkosa,Amissi Tambwe, Obrey Chirwa,  Thaban Kamusoko na Donald Ngoma pamoja.

Tambwe ambaye ni mchezaji wa yanga na amewahi kutamba na Simba amesema “Yanga hawana haja ya kuwa na wasiwasi na wache­zaji watakaocheza dhidi ya St Louis, kwani ni wachezaji wa­zuri na wana uwezo wa kufanya vizuri endapo wataamua kupambana"
AJIRA KWA WOTE ZIMEPATIKANA KWA WASOMI WA TANZANIA

PROCUREMENT AND LOGISTIC OFFICER
Qualifications : Holder of a Bachelor degree in Business Administration,Procurement and Logistics Management or any other Bachelor degree in Procurement related field
Apply: The General Manager,
National Ranching Company Limited
Box 9113 , Dar es Salaam
Details: Daily News Febr  7, 2018 
Deadline: March  02, 2018

MANAGER INTERNAL AUDIT
Qualifications : Holder of a Master degree in Business Administration,or relevant field,he/she should be registered with NBAA as CPA 9T) and shall have at least seven years working experience in the Audit field
Apply: The General Manager,
National Ranching Company Limited
Box 9113 , Dar es Salaam
Details: Daily News Febr  7, 2018 
Deadline: March  02, 2018

MARKETING AND PUBLIC
RELATIONS OFFICER
Qualifications : Holder of a Bachelor degree in Marketing and/or Public relations and shall have at least five years working experience in the marketing or Public relations field
Apply: The General Manager,
National Ranching Company Limited
Box 9113 , Dar es Salaam
Details: Daily News Febr  7, 2018 
Deadline: March  02, 2018

PRODUCTION MANAGER
Qualifications : Holder of a Bachelor degree in Manufacturing/Industrial Engineering,Mechanical Engineering,Electrical Engineering or Chemical and Processing Engineering and a Holder of Master degree in Business related field
Apply: The General Manager,
National Ranching Company Limited
Box 9113 , Dar es Salaam
Details: Daily News Febr  7, 2018 
Deadline: March  02, 2018

DRIVER II - 2 POSITIONS
Qualifications : Holder of Certificate of secondary Education with passes in Kiswahili and English must have a valid class C driving license of not less than three years without causing accident and should posses Trade Test Grade III or above/drivers Grade II Certificate from a recognized Training
Apply: Director General Sugar Board of Tanzania
Box 4355, Dar es Salaam
Details: Daily News Feb. 08, 2018 
Deadline: February  23, 2018

SENIOR RANCH ASSISTANT GRADE II
Qualifications : Form IV/VI who has three years satisfactory services in that Grade. Must have  acquired a Certificate in veterinary Sciences,range Management,or General
Husbandry from a recognized institution
Apply: The General Manager,
National Ranching Company Limited
Box 9113 , Dar es Salaam
Details: Daily News Febr  7, 2018 
Deadline: March  02, 2018

FIELD OFFICER GRADE II - 4
POSITIONS
Qualifications : Holder of a Form IV/Form  VI Certificate plus a Diploma in veterinary Science,or Ranch Management or Animal Husbandry or range Management from a recognized institution with at least three years of working experience
Apply: The General Manager,
National Ranching Company Limited
Box 9113 , Dar es Salaam
Details: Daily News Febr  7, 2018 
Deadline: March  02, 2018

ACCOUNTS ASSISTANT GRADE II
Qualifications : Form IV/VI,ATEC II/Ordinary Diploma with working experience of three years
Apply: The General Manager,
National Ranching Company Limited
Box 9113 , Dar es Salaam
Details: Daily News Febr  7, 2018 
Deadline: March  02, 2018

ACCOUNTANT GRADE II - 2 POSTS
Qualifications : Advanced Diploma or equivalent,who has successfully completed at least three years service in that grade ,who has acquired ATEC II/I or equivalent
Apply: The General Manager,
National Ranching Company Limited
Box 9113 , Dar es Salaam
Details: Daily News Febr  7, 2018 
Deadline: March  02, 2018

AIR NAVIGATION ENGINEER II - 6 POSITIONS
Qualifications : Holder of Bachelor degree in Engineering majoring in Telecommunication or Electronics or its equivalent professional qualification from ICAO recognized institution that will undergo a CNS induction course and CNS equipment concept Course. Must be registered as a Graduate Engineer
Apply: Director General Tanzania Civil Aviation Authority
Box 2819 , Dar es Salaam
Details: Mwananchi
February  9, 2018 
Deadline: February  22, 2018

MARKETING OFFICER GRADE I
Qualifications : Holder of a degree in Marketing or equivalent or Commerce,Business Administration or Economics with bias in Marketing or equivalent who has three years satisfactory service in that Grade
Apply: The General Manager,
National Ranching Company Limited
Box 9113 , Dar es Salaam
Details: Daily News Febr  7, 2018 
Deadline: March  02, 2018

VETERINARY OFFICER I
Qualifications : Holder of a degree in veterinary Science/Veterinary Medicine with a working experience of not less than three years in this field and registered as a Veterinary
Apply: The General Manager,
National Ranching Company Limited
Box 9113 , Dar es Salaam
Details: Daily News Febr  7, 2018 
Deadline: March  02, 2018

OFFICE ASSISTANT II - 2 POSTS
Qualifications : Secondary of School Education with passes in Kiswahili and English languages
Apply: Civil Aviation Authority,
Zanzibar International Airport
Box 1061 , Zanzibar
Details: Mwananchi Febr  9, 2018 
Deadline: February  22, 2018

DRIVER II
Qualifications : Certificate of Secondary School Education with passes in Kiswahili and English,Class C,C1,C2, and C3 valid driving license and Trade Test Certificate from a recognized institution
Apply: Civil Aviation Authority,
Tabora Airport
Box 164 , Tabora
Details: Mwananchi Feb 9, 2018 
Deadline: February  22, 2018

ELECTRICAL TECHNICIAN I
Qualifications : Ordinary Diploma in Electrical Engineering from a recognized institution or equivalent qualification with a working experience of not less than three years in the relevant field
Apply: Director General Tanzania Civil Aviation Authority
Box 2819 , Dar es Salaam
Details: Mwananchi
February  9, 2018 
Deadline: February  22, 2018

MANAGING DIRECTOR
Qualifications : Holder of a Master degree in Industrial Engineering,Business Administration,Finance,Economics,Public Administration or related fields from a recognized institution and shall have at least 10 years
Apply: The General Manager,
National Ranching Company Limited
Box 9113 , Dar es Salaam
Details: Daily News Febr  7, 2018 
Deadline: March  02, 2018




Jumanne, 20 Februari 2018

Mtumishi wa TRA alawiti mtoto wa kiume wa miaka 13

Mtumishi wa TRA anashikiliwa na Jeshi la Polisi la Visiwani Zanzibar kwa kosa la kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 13.
Jeshi la Polisi la Visiwani Zanzibar linamshikilia mtumishi mmoja wa TRA aitwaye Hassan AboudTwalib kwa jina maarufu KIRINGO kwa kosa la kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 13.
Inadaiwa mtuhumiwa alimfanyia kitendo hicho cha kinyama mtoto huyo baada ya kumpeleka katika nyumba ambayo haijamaliza kujengwa iliyopo eneo la fuoni uwandani(Unguja) kisha kumpa madawa ya kupoteza fahamu na kumfanyia unyama huo.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa mnamo tarehe 18 Februari 2018 akiwa katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Aman visiwani humo akitaka kusafiri kuelekea mkoani Mwanza.Alikamatwa baada ya baba wa mtoto huyo kuripoti tukio hilo kituo cha polisi.
 KOCHA MCHEZAJI KING KIBADENI AFUNGUKA HAYA

KOCHA na mche­zaji wa zamani wa Simba, Abdallah Kibadeni ‘King Kibadeni’, amefunguka kuwa kama Simba itaendelea na moto ilionao, basi ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, tofauti na wapinzani wao Yanga ambao wa­naonekana kuchoka. 

“Ligi ya msimu huu imekuwa ngumu na ushindani mkubwa kwa timu zote lakini kwa hizi timu za juu yaani Simba na Yanga kila moja inaonekana inapambana vilivyo, ila binafsi naona Simba wapo kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuweza kutwaa ubingwa tofauti na Yanga.

“Lakini haitakuwa rahisi kama hawataweza kuendelea na kasi am­bayo wanayo hivi sasa, kwa sababu ukiangalia wameweza kushinda michezo mingi kwa mabao ya kuto­sha na ukiwaangalia Yanga wa sa­fari hii ni wazi hawapo vizuri kama tulivyozoea,” alisema Kibadeni wakati anahojiwa na waandishi wa habari

Jumamosi, 17 Februari 2018

Alichokisema Hussein Bashe baada Ya Tukio la Mwanafunzi Kupigwa risasi Cha Shitua Wengi

Huu ni Unyama, Binti huyu hakua na kosa hakua na dhambi kama Tume ya Uchaguzi ingetoa Viapo vya Vyama mapema kusingetokea Maandamano na Vurugu kupelekea Binti huyu kufatiki
Ndoto zake Ndoto za Familia yake Ndoto za Rafiki zake zote zimepotea ,Tukiwa Tandale kigogo Ndugumbi Magomeni Tulisema Tume Itende Haki kwa Vyama vyote
Tukio hili la Mauwaji Tukio la Mauwaji la Kiongozi wa Chadema ndg Daniel ni matukio ambayo Lazima ipatikane Indipendent investigation haiwezekanj By election zote Mauwaji yanatokea hakuna anaefikishwa mbele ya Vyombo vya dola Hatuwezi kujenga Nchi bila Haki na wajibu ,Hatuwezi kujenga Nchi bila kulinda UHAI wa Mtanzania Kila Mtanzania lazima alindwe na uhuru wake ulindwe
Jambo hili si la Chadema si La CCM si la kwetu wa Wana Siasa jambo hili ni la watanzania wote lazima sote tuungane kudai Alietoa Uhai wa Binti huyu apatikane
Hili ni Jambo ambalo la kulaani
Mambo Matatu aliyozungumza Rafiki wa karibu wa Mwanafunzi aliyepigwa Risasi


Leo February 17, 2018 Rafiki wa Karibu wa Mwanafunzi wa Chuo cha NIT aliyepigwa Risasi February 16, 2018 Aquillina Akwilini ameongea na AyoTV na millardayo.com ambapo ameelezea alikokuwa na anaenda rafiki na nini kinaendelea mpaka sasa. aliongea kwa uchungu sana kumpoteza kipenzi chake bonyz play hap chn kuangalia mahojiani yote na usisite kutoa maoni yako

Baada Ya Diamond Kulia Sana Jana, Zari Amlipua Diamond


Ikiwa leo ni siku ya tatu toka Zari atangaze rasmi kuachana na mzazi mwenzake Diamond Platnumz kupitia ukurasa wake wa instagram, Leo February 17,2018 kupitia mtandao wa Snapchat wa Zari ameandika caption ambayo inatafsirika ni ujumbe kwa Diamond Platnumz.
Zari the boss lady ameandika “Utakoma tu mwenzangu” akiwa anaangalia wimbo wa Sikomi wa Diamond Platnumz kwenye Tv.

Polisi Yakiri Kumpiga risasi Mwanafunzi kwa bahati mbaya, Yatowa Huu Ufafanuzi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amekiri kuwa mtu mmoja alipigwa risasi na polisi kwa bahati mbaya wakati wakiwatawanya wafuasi wa Chadema walioandama jana Februari 16, 2018, jioni. Wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wafuasi hao waliandamana kuelekea ofisi ya msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Kinondoni

Alhamisi, 15 Februari 2018

Maneno Ya Harmonize baada Ya Zari Kumuacha Diamond Yafichua siri Nzito Kumbe ndo mchezo wao

February 14, 2018 mitandao ya kijamii ilichangamka sana baada ya post ya mzazi mwenza na Diamond Platnumz, Zari the Boss Lady kupost ua na ujumbe mzito wa kuachana na Diamond kitu ambacho baadae Harmonize amekuja kupost video fupi ya utani kuhusu hilo.
Harmonize amepost video hiyo inayomuonesha akiwa kwenye chumba cha kulala na mwanamke huku akiimba wimbo wa kuachwa na kisha kwenda kwenye ua huku akiliambia lile ua lisije kubadilika likawa jeusi, hata hivyo zari alipost ua lililobadilika rangi kutoka jekundu na kuwa jeusi.


Abdukiba kafunguka “Mimi Ndio Niliomla Tunda Mara nyingi Kuliko yeyote, ila kitandan….

  Msanii Abdukiba ambaye ana undugu wa damu na msanii Alikiba amezungumza kwa mara ya kwanza na kuelezea ukweli kuwa alishawahi kutoka na Tunda kwenye uhusiano wa kimapenzi, Hii imekuja baada ya kumuuliza swali kuwa ni uhusiano upi katika maisha yake anaumiss sana ndipo akamtaja Tunda na kueleza ilivyokuwa wakati wakiwa pamoja na kwanini hawakutaka kuyaweka mahusiano yao public na ipi ni sababu ya wao kuachana..? Bonyeza PLAY hapa chini kumtazama ABDUKIBA akielezea FULL STORY

MSANII TID ASEMA MAKONDA AMENIPONZA,SOMA HAPO KUJUA

Msanii wa muziki, TID amelalamika kuwa baadhi ya watu wanamfanyia figisu figisu ili asipate show kutokana na ukaribu wake na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Muimbaji huyo amefunguka hayo katika kipindi cha Eight cha TVE kwa kudai kuwa hali hiyo inampa tabu sana.

“Kuna watu wananibania kupata dili, wengine wanaenda mpaka kwa waandaaji sipati show. Napata dabu kweli,” amesema TID.


TID ameongeza kuwa Mhe. Makonda ni mtu ambaye yuko poa sana na watu na kila anachokifanya anakuwa na uhakika nacho.
Hii Ndio List ya ‘Michepuko’ aliyoipitia Diamond wakati yupo na Zari!

Habari za Diamond na Zari kuachana bado zinatawala kwenye mitandao ya kijamii huku wengi wakiwa wameshtushwa kusikia kuwa couple iliyokuwa inapendwa na mashabiki zao imevinjika.
Baadhi ya michepuko ambayo inasemekana kuchangia kuvunja uhusiano wa Diamond na Zari ni hawa hapa:
1. Hamisa Mobetto
2. Irene / Officiallyn Irene na Diamond wametajwa kuwa na mahusiano kwa muda mrefu sana tangu alipotokea kwenye video ya kwetu ya Rayvanny
3. Shady Huyu ni mwanamitindo kutoka nchini Rwanda
4. Mia Mwezi uliopita kuna video ilisambaa mtandaoni ambayo ilimuonyesha Mia akiwa Madale
5. Tunda huyu anajulikana
6. Wema Sepetu alikuwa anakuja madale kila weekend
Mbasha Aitikisa Ndoa ya Masanja, hali mbaya jione mwenyewe Hapa


Kisa kikidaiwa kuwa ni penzi la Miss Tanzania 2008, Jacqueline Chuwa ‘Jack’, muimbaji wa nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha ameitikisa ndoa ya Mchekeshaji Emmanuel Masanja ‘Mkandamizaji’ baada ya kuchukua picha ya Masanja aliyopiga na miss huyo kisha kuipamba na maneno ya kichochezi.
Picha hiyo Mbasha aliitupia kwenye Mtandao wa Instagram kitendo kilichosababisha hali ya hewa kuchafuka kwa saa kadhaa kwani wapo waliomshambulia Masanja lakini wengine walimshambulia yeye mwenyewe.
Mbasha aliipamba picha hiyo ya Masanja na Jacqueline kwa kusindikiza na ujumbe uliosomeka hivi:
“Kweli ndoa ni pingu aisee… uvumilivu umemshinda mshikaji wangu kaona cha kufia…isiwe shida. Kamposti X wake. Imekaa poa au? Kama namuona Monika (mke wa Masanja) anavyoiangalia hii picha.”
Mtoto wa Kitanzania arudishwa nchini baada wazazi wake kuhukumiwa kifo China.

Raia wawili wa Tanzania, Baraka Malali na mkewe Ashura Mussa walikamatwa nchini China Jan. 19 mwaka huu kwenye uwanja wa ndege wa Baiyun Guangzhou, wakiwa wamemeza tumboni dawa za kulevya, walihifadhiwa kwenye chumba maalum kwa muda Baraka alitoa pipi 47 kwa njia ya haja ambapo mkewe alitoa pipi 82.

     Watuhumiwa hao walikatwa wakiwa wameandama na mtoto wao mwenye umri wa miaka 2 na miezi 9. Serikali ya China iliwasiliana na serikali ya Tanzania kuhusiana na suala la mtoto huyo ambapo walikubaliana kumrudisha mtoto huyo nchini, mtoto huyo alitarajiwa kuingia nchini leo saa saba mchana akiwa ameambatana na Afisa wa wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda.
     Serikali kupitia Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya na Ustawi wa Jamii inafanya jitihada za kuwasiliana na ndugu na jamaa wa watuhumiwa ili kuhakikisha mtoto huyo anakabidhiwa kwao kwa jaili ya malezi na matunzo.

Machapisho Maarufu