Nchini India mwanamke mmoja ajulikanaye kwa jina la Rajashree Patil, 49, ambaye miaka miwili iliyopita alifiwa na mtoto wake wa kiume wa pekee aliyekuwa anaumwa saratani ya ubongo.
Kutokana na kushindwa kumsahau mwanaye na kukubaliana na ukweli wa
kuishi maisha bila mwanaye huyo mama huyo aliamua kwenda kuomba mbegu za
kiume za mwanaye huyo ambazo zilikuwa zimehifadhiwa hospitalini.
Alimtafuta mwanamke mmoja na kumuomba amlipe ili apandikizwe mbegu hizo za mwanaye na ashike ujauzito (surrogate) ili tu amzalie wajukuu ambao anaamini wataziba pengo la mwanaye huyo.
Habari njema ni kwamba mwanamke huyo amefanikiwa kujifungua watoto
mapacha siku za hivi karibuni. Pacha hao ambao ni wa kike na wa kiume
wamepewa majina ya Prathamesh na Preesha.
0 maoni: