Siku ya leo wakazi wa kata ya Tomondo wilayani Morogoro jimbo la Morogoro kusini Mashariki mambo yao ni motoooo baada ya kupata ufumbuzi wa baadhi ya kero za miradi yao mbalimbali ya maendeleo
Kata hiyo inayoongozwa na Diwani wa Chama cha ACT Wazalendo, Hamisi Msangule February 21, 2018 ilitembelewa na viongozi wa chama hicho ngazi ya Taifa, Mkoa na Jimbo ambao waliwezesha kutatua baadhi ya changamoto.
Changamoto kubwa ambayo imepewa
kipaumbele kutatuliwa na chama hicho ni kero ya maji inayowakabili
wakazi wa kata hiyo ambayo chama hicho kimeahidi kuwapeleka wataalamu wa
kutoboa visima virefu kwenye kila Kijiji ndani ya mwezi huu.
Akiwa kwenye kikao cha ndani na wananchi wa kata hiyo mwenyekiti wa chama cha ACT kitaifa , Zitto Kabwe aliwaambia wananchi hao kama watashindwa kumaliza kero hiyo haitakuwa na maana tena chama hicho kupewa dhamana tena kuongoza.
“Chama
chetu ni tofauti sana na vyama vingine, tunafanya siasa za maendeleo
kwa ushirikishaji wananchi katika kutatua changamoto zao,” -Zitto Kabwe
0 maoni: