Tafuta katika Blogu Hii

Jumatano, 21 Februari 2018

MKUU WA WILAYA AMRUHUSU MUMEWE KUOA MKE WA PILI

Leo watumizi wa mitandao ya kijamii walipigwa na bumbuwazi baada ya kuona post iliyo kwenye ukurasa wa instagram (@zainabuabdallah93) ya Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainab Abdallah akitoa pongezi kwa Mume wake baada ya kuoa mke wa Pili. Watu wengi walijikuna sikio huku wakibakli mdomo wazi, kwani ni nadra sana kuonaMwanamke mwenye cheo kikubwa na wadhifa wa kutosha akimpongeza Mumewe kwa kuongeza mke

Kupitia ukurasa wake wa instagram mkuu wa wilaya ya pangani ameandika 
kuwa wazo la mume wake kuongeza mke wa pili lilitoka kwake, baada ya kuona majukumu ya kazi yanambana na kushindwa kutekeleza majukumu ya ndoa.

Nichukue nafasi hii kumpongeza Mume wangu  kwa kuongeza mke wa pili. Kwa kuwa dini yetu ya Kiislam inaruhusu, wazo la kufanya hivyo lilitoka kwangu, kulingana na uzito wa majukumu yangu nalazimika mda mwingi kuwa mbali na nyumbani na hivyo mume wangu kukosa huduma za msingi” -DC Zainab 
”Namshukuru kwa kunielewa na kulifanyia kazi ombi langu, hatimaye nimempata mwenzangu wa kusaidiana naye majukumu mazito ya ulezi wa mume. Alhamdulillah, M/Mungu ametupa riziki na uwezo, hivyo tunapaswa kutumia neema hizi na wengine. Mavazi ya mume wangu nimeyaandaa mwenyewe, yaa rabb atupe stara inshaaAllah.” DC Zainab

0 maoni:

Machapisho Maarufu