Tafuta katika Blogu Hii

Jumanne, 27 Februari 2018

RAIS ACHAGUWA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI


Usiku wa jana, February 27,2018 Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa ametangaza baraza lake jipya la Mawaziri ikiwa ni baada ya kuchukua madaraka kutoka kwa Jaco Zuma.

Baadhi ya mawaziri walioteuliwa ni  Nhlanhla Nene aliyekuwa Waziri wa zamani wa fedha. Nene alifukuzwa  kazi December, 2015 na Rais wa zamani Jacob Zuma na nafasi yake ikachukuliwa na Des van Rooyen.
 
Baada anguko la thamani ya randi, Zuma alilazimika kumfukuza kazi Rooyen na kumteua Pravin Gordhan, siku nne baadae ambaye pia alimfukuza kazi baadae. Katika baraza la Ramaphosa, Gordhan amerejea kama waziri wa masuala la biashara.

0 maoni:

Machapisho Maarufu