Tafuta katika Blogu Hii

Jumanne, 20 Februari 2018

Mtumishi wa TRA alawiti mtoto wa kiume wa miaka 13


Mtumishi wa TRA anashikiliwa na Jeshi la Polisi la Visiwani Zanzibar kwa kosa la kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 13.
Jeshi la Polisi la Visiwani Zanzibar linamshikilia mtumishi mmoja wa TRA aitwaye Hassan AboudTwalib kwa jina maarufu KIRINGO kwa kosa la kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 13.
Inadaiwa mtuhumiwa alimfanyia kitendo hicho cha kinyama mtoto huyo baada ya kumpeleka katika nyumba ambayo haijamaliza kujengwa iliyopo eneo la fuoni uwandani(Unguja) kisha kumpa madawa ya kupoteza fahamu na kumfanyia unyama huo.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa mnamo tarehe 18 Februari 2018 akiwa katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Aman visiwani humo akitaka kusafiri kuelekea mkoani Mwanza.Alikamatwa baada ya baba wa mtoto huyo kuripoti tukio hilo kituo cha polisi.

0 maoni:

Machapisho Maarufu