Tafuta katika Blogu Hii

Ijumaa, 23 Februari 2018

SHILOLE ASEMA KUMPIGA MAKOFI MPENZI WAKO NI MAHABA NIUWE

MSANII Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ambaye ameolewa hivi karibuni na mzee baba Uchebe amesema katika maisha yake ya ndoa na mumewe Uchebe hajawahi kumpiga makofi.

Kauli hiyo Shilole aliitoa juzi alipofanyiwa mahojiano na Enews ya EATV ambapo aliulizwa kama atampiga makofi mumewe kama alivyofanya kwa wanaume waliotangulia kabla ya kuolewa.

“Tabia hiyo nimeacha na ule ulikuwa utoto siwezi kumpiga Uchebe kwani ni mwanaume anayejiamini na jasiri pia ana misimamo yake”.

“Nikimpiga yatakuwa makofi ya chumbani ambayo mtu na mpenzi wake wanafanya kimahaba, si unajua yule alikuwa anapigana (bondia) na ana mkanda,” aliongeza Shilole.

Shilole aliwahi kumpiga makofi aliyekuwa mpenzi wake Nuh Mziwanda kabla ya kuachana.

0 maoni:

Machapisho Maarufu