Idara ya Uhamiaji nchini inawashikilia watanzania 9, ambao ni
wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala(KIU) jijini Dar es
Saalam kwa kutokuruhusu maofisa wa idara uhamiaji kufanya kazi yao
walipofika chuoni hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari Msemaji wa Idara ya Uhamiaji Ally Mtanda amesema watu 9 washikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kuzua chombo kinachohusika na uhamiaji wasitimize adhima yao.
"Watu hao baada ya maofisa wetu jana kufika pale KIU
waliamua kuwazuia kwa kufunga milango ili tusipate nafasi ya kufanya
kile ambacho kimetupeleka,"amesema.
Kukamatwa kwa watu hao kunafanya idadi ya wanaowashikiliwa na Idara ya Uhamiaji kufikia 48.
"Idara ya Uhamiaji inaendelea kuwahoji na kati ya hao
wanaoshikiliwa wapo raia wa Nigeria watano, raia wa Congo mmoja, raia wa
Uganda 30, raia wa Kenya 3 pamoja na hao raia wa Tanzania 9,"amesema.
Amefafanua Idara ya Uhamiaji itaendelea kukagua vyuo mbalimbali
nchini kwani ni agizo la Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
0 maoni: