ZITTO KABWE CHINI YA MIKONO YA POLISI
Mbunge wa Kigoma Mjini na Mwenyekiti wa taifa wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe jana February 22, 2018 ameshikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo cha Polisi cha Mgeta wilayani Mvomero, Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya mahojiano.
Zitto kwa sasa yupo katika ziara ya mikoa mbalimbali kwa ajili ya kukagua na kuimarisha uhai wa chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari jana alhamisi February 22,2017 amesema ametakiwa kuripoti katika kituo hicho baada mkuu wa polisi wa wilaya (OCD) kuagiza aende.
"ninapozungumza na nyinyi naelekea kituo cha polisi na gari yangu ipo mbele ya polisi na sijajua kosa langu ni nini" amesema Zitto.
Waandishi wa habari walipo jaribu kuzungumza na Katibu Kamati ya Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa ACT Wazalendo Ado Shaibu alisema mpaka sasa bado yupo anashikiliwa na Polisi hawajui ni kosa gani ambalo Zitto Kabwe limefanya akamatwe.
Nae Wakili wa Zitto Kabwe, Emmanuel Lazarus Mvula alisema jalada la mashataka dhidi yake limefunguliwa katika kituo cha Polisi Mgeta.
“Hivi Sasa saa 3.30 usiku ndugu Zitto amechukuliwa na OC-CID na polisi wenye silaha anapelekwa Kituo cha Polisi cha Wilaya, cha Dakawa ili kuandika maelezo kwasababu hakuna umeme katika kituo cha Polisi Mgeta”
0 maoni: